Mkuu wa chuo cha afya Hermargs Mr.Benedict Lugwisha,akitoa utambulisho kwa wageni waliohudhuria katika hafla ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza wa kozi ya famasia mwaka 2021/2022

Mkurugenzi wa Hermargs Mdegela Academy Limited(Prof.Robinson Mdegela) akikabidhi zawadi kwa Bi.Paskalina John kwa mchango wakukitangaza chuo nq kuleta wanafunzi wawili.

Mwinjilisti Bw.Mwinuka akizungumza machache na wanafunzi huku akiwakumbusha maneno ya bibla kutoka kitabu cha mithali 4:13 ( mshike sana elimu usimuache aende zake)

Mkurugenzi wa chuo Prof.Mdegela akitoa neno fupi Kwa wanafunzi huku akigusia mstali wa bibla katika kitabu cha kutoka 14:14( Bwana atawapigania ninyi,nanyi nanyi mtanyamaza kimya

Mkuu wa chuo pamoja na wageni waalikwa wakiingia ukumbini

Mkuu wa chuo akitoa neno fupi kwa wanafunzi,akiwasisitizia kuwa na nidhamu,kujituma na kuwajibika ipasavyo ilikufikia ndoto zao.

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaokaribishwa wakiwa na nyuso za furaha huku wakiwapungia mikono wageni waliopo ukumbini.

Mkurugenzi msaidizi wa chuo Prof Helena Ngowi akitoa neno fupi la shukrani kwa wageni wote na watu wote waliohudhuria.
